Habari
Uti aula Dola Laki Mbili
Mshindi wa Big Brother Africa All Stars ametajwa kuwa Uti kutoka Nigeria.
Ushindi huu umekuwa ni wa bahati na wa kustaajabisha sana baada ya fainali kuwa yeye Uti na Munya kutoka Zimbabwe, mshindani aliyekuwa amesadikika kushinda shindano hili na wengi.
Ingawa mshindani kutoka Tanzania, Mwisho Mwampamba hakufanuikiwa kutwaa fedha hizo, alipata nafasi ya kuingia kwenye tano bora za mashindano hayo pamoja na Sheila kutoka Kenya, Lertao kutoka South Africa pamoja na Uti na Munya.
Bongo 5 inamtakia Uti kila la kheri kwenye maisha yake yaliyoongezeka dola laki mbili!