Burudani
Mense ajitoa Mexicana
Producer na mwanamuziki aliyekuwa akitengeza kazi za kundi la Mexicana Lacavera Mensen Selecter amejitoa rasmi kwenye kundi hilo, na kuwa msanii pekee anayejitegemea.
Mwanamuziki huyo na ndiye aliyeanzisha kundi hilo wakiwa watatu pamoja na Klimax… Kiongozi wa kundi hilo Praygod ‘Baghidad’ amesema kweli mwanamuziki huyo ametoka kwenye kundi hilo, na wanamuombea safari ndefu ya kimuziki na wanampa baraka zote.
Baghad amesema pia kwa sasa wanaweza kufanya kazi zao kwenye studio tofauti tofauti kwakuwa mwanzo walikuwa wakifanya kazi zao zote kwa Producer huyo aliyedondosha kitu kama Kumpadupa, ona na nyingine nyingi.