Burudani
Nilitaka kumzuia asishiriki
Baba mzazi wa Miss Tanzania 2010, Genevieve Mpangala, Emmanuel Mpangala ambaye ni Meneja wa timu ya Yanga amesema nusura amzuie mwanae kushiriki mashindano hayo kutokana na hofu kuwa ataharibikiwa.
Mpangala alimpongeza mwanae kwa ushindi huo “Nilikuwa sitaki lakini baadaye mimi na mama yake tuliamua kumruhusu na kumpa baraka zote”.
“Najua kwa sasa ameingia katika ulimwengu wa watu maarufu hivyo atakuwa anamulikwa na vyombo vya habari, naamini ataendelea kuwa mwema katika jamii. Nasi wazazi tutaendelea kumshauri juu ya maisha yake mapya” alisema Mpangala.
Mpangala ametangaza kumpa Genevieve zawadi ya nyumba anayomiliki iliyo katika kitongoji maarufu cha jiji la Dar es Salaam.