Michezo

Abdi Banda asimamishwa kucheza ligi kuu Tanzania bara

Mchezaji wa klabu ya Simba Abdi Banda amesimamishwa kucheza mechi za Ligi Kuu wakati akisubiri suala lake la kumpiga ngumi kiungo wa Kagera Sugar,George Kavilla wakati hana mpira kusikilizwa na kutolewa uamuzi na kamati ya Nidhamu ya TFF.

Maamuzi haya yamekuja baada ya kamati ya usimamizi na Uendeshaji wa Ligi Tanzania au kamati ya Saa 72 kufanya kikao chake siku ya ijumaa April,7,2017 jijini Dsm.

Banda alifanya tukio hilo April 2,2017 kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar katika uwanja wa Kaitaba ambapo mwamuzi hakuona tukio hilo. Simba ilipokea kichapo cha 2-1 katika mchezo huo.

Pia kamati hiyo ilibaini kuwa Abdi Banda alifanya kitendo kama hicho kwenye mchezo kati ya Simba na Yanga uliopigwa Uwanja wa Taifa,Dsm Feb 25,2017.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents