Habari

Abdul Kiba adai wimbo ‘Ayaya’ alikuwa amshirikishe Vanessa Mdee ila ikashindikana

Abdul Kiba amesema kabla ya kufikiria kufanya wimbo wake wa ‘Ayaya’ na Ruby alipanga kumshirikisha Vanessa Mdee.

12120284_547285642095436_1812220108_n

Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds TV kuwa, Vanessa alimuacha njia panda kwa muda mrefu bila kumjibu ndio maan akaamua kufanya na Ruby.

“Kwanza nili-plan kufanya wimbo na Vanessa, nilimtumia ule wimbo wakati umetimia wote kwa sababu niliweza kuutunga wote, akausikia ila ilishindikana kufanya kwa sababu process zake zilikuwa nyingi,” alisema. “Kwanza alikuwa busy na kazi zake, mara ana safari kwenda nje ya nchi, so na mimi time ilikuwa inanibana, mashabiki wanahitaji kazi kutoka kwangu kwahiyo nikaona kwa nini nimsubiri sana wakati nina deni kwa mashabiki! Baada ya kuona Vanessa hana jibu analonipa, mimi ilinibidi nimtumie Ruby aweze kuusikia kwa sababu kuna mistari ambayo niliiweka na ilikuwa inastahili mtoto wa kike aimbe,” aliongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents