Burudani

Afande Sele anaamini kuwa muziki wa Tanzania ulizaliwa Morogoro

Afande Sele anaamini kuwa asili ya muziki wa Tanzania ni Morogoro na Songea.

Afande-Sele-nzuri_full

Kauli hiyo aliitoa kwenye 255 ya kipindi cha XXL cha Clouds FM.

“Unajua Morogoro imeingiliana kwa karibu sana Songea,” alisema.

“Ukienda Malinyi,Ulanga unakuta Songea ipo karibu sana na ukizungumzia suala la muziki Morogoro ni kama umepita lakini umetokea nyanda za juu kusini maana Waruguru pia asili yao imetokea kule wakajigawanyagawanya. Kama unakumbuka historia ya Waruguru, walitokea Kusini wakaenda Songea wakafika hadi Iringa na asili ya jina Morogoro ni mgogoro baada ya kutokea huko kusini ndo wakakimbilia huku. Muziki asili yake ni nyanda za juu kusini,” aliongeza.

“Palikuwa na ngoma kama Sangula ambazo zimetoka kule ambazo ziliasisi muziki, ngoma pia kama Mdundiko na Mkwaju ngoma ambazo tune yake ni ya muziki kabisa. Ndio maana unakuta wasanii wa zamani walianzia kuimba nyimbo za kienyeji na kupiga ngoma. Ndio maana akina Mbaraka Mwishehe na Salum Abdalah walikuta tayari palikuwa na wasanii wakubwa ambao walikuwa wanaimba kupitia nyimbo za asili ambazo zilikuwa pale tu Morogoro. Ndio maana nasema muziki ulianzia hapa.”

Unakubaliana na maneno ya Afande?

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents