Burudani

Godfather kuongoza video ya Yamoto Band, Diamond aigharamia

Muongozaji wa video za muziki wa Afrika Kusini, Godfather ataongoza video ya wimbo mpya wa kundi la Yamond Band ‘Cheza Kimadoido’ na Diamond ndiye atakayeigharamikia.

yamoto

Meneja wa kundi hilo, Said Fella, amesema Yamoto Band watasafiri Jumatatu kuelekea nchini Afrika Kusini kushoot video hiyo.

“Wiki ijayo tunatarajia kufanya video mpya ya Yamoto Band na Godfather atakuwa director,” Fella ameiambia Bongo5. “Hatuendi south kama kuiga lakini madogo nao wanataka kwenda mbali zaidi.”

“Tunajaribu kuwapenyeza zaidi Afrika. Kwahiyo Diamond ndio kaongea na Godfather na yeye ndo katoa hiyo ofa, hivyo hii ni ofa ya Nasib. Tunakwenda Jumatatu, tunafanya video Jumanne na Jumatano kuna shughuli tutaifanya tena,” alisema Fella.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents