Habari

Aliyekamatwa kwa kosa la uzururaji aiomba Mahakama imfunge

Kwa jinsi hali ya uchumi inavyobana tutaendelea kujionea mengi hapa duniani. Mwanaume mmoja nchini Uingereza amejikuta akimuomba jaji mahakamani amfunge jela baada kukutwa na kosa la uzururaji.

Bradley Grimes

Mwanaume huyo aliyetambulika kwa jina la Bradley Grimes (23) alimuomba jaji wa mahakama ampeleke gerezani kuliko kumuacha kurudi uraiani kutumikia adhabu aliyopewa mahakamani hapo ya kufanya usafi kwenye maeneo ya umma.

Nilijaribu kumuomba jaji Mahakamani anifunge gerezani kuliko kunipa adhabu ya kunirudisha uraiani niendelee kuteseka kwa kuomba omba na kulala nje ya maduka ya watu.“amesema Grimes kwenye mahojiano yake na BBC.

Hata hivyo kwenye maelezo yake aliyotoa, Grimes amesema alianza kuishi maisha ya kutanga tanga baada ya kuondoka kwenye nyumba za watoto wenye mahitaji maalumu akiwa na umri wa miaka 17.

Bradley Grimes ambaye anatatizo la kigugumizi amesema alitafuta kazi kila kona mjini Middlesbrough ili kujikimu na maisha lakini hakufanikiwa ndipo alipoamua kuanza kazi ya kuzurura na kuomba omba kwenye maduka mjini humo.

Akielezea safari ya maisha yake ya kuomba kuomba na kulala nje ya maduka, Grimes amesema alikuwa akishikwa kila wiki kwani kila sehemu aliyokuwa analala kulikuwa na CCTV Kamera ambazo zilituma picha moja kwa moja kwa Polisi kwa ajili ya usalama.

Yaani nimekuwa zaidi ya mfungwa, nimekuwa nikikamatwa kila wiki. Unajua kwenye maduka nje kumefungwa mitambo ya CCTV Kamera ambazo zinachukua picha na kuituma moja kwa moja kwa polisi na walinzi wa mitaa. Polisi wakija, unakamatwa. Yani nashindwa kukaa sehemu moja kwa kuhofia kukamatwa na polisi ndio maana nimekuwa mzururaji.“ameeleza Grimes.

Grimes alikamatwa wikiendi iliyopita kwa makosa ya kuzurura na kukiuka hukumu ya kifungo cha nyumbani cha miezi minne kosa ambalo alikiri kulifanya na alimuomba Jaji kumfunga jela ili kumuondolea matatizo anayoyapata uraiani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents