Habari

Wazazi watakiwa kuacha tabia ya kuwatolea lugha zisizofaa Watoto wanaofeli mitihani

WAZAZI na walezi nchini wamesisitizwa kuacha tabia ya kuwatolea lugha zisizofaa watoto wao wanaofeli mitihani yao hasa ya kitaifa na kuwaonesha kuwa hawawezi.

Rai hiyo imetolewa na Mwasisi wa Shule ya Sekondari Huria ya Skillful, Diodorus Tabaro wakati wa Mahafali ya 18 ya Kidato cha Sita, yaliyofanyika shuleni hapo Ukonga ambapo wanafunzi 75 wanatarajiwa kufanya mitihani ya kuhitimu.

Tabaro alisema ni vyema mzazi kutumia lugha rafiki kwa watoto wanaofeli mitihani yao pamoja na kutafuta njia ya kumsaidia ikiwemo kumtafutia shule Huria ili aweze kuendelea kusoma na hatimaye kufikia malengo yake.

“Wazazi waepuke kuwanenea mabaya watoto wao. Kuna wazazi ambao mtoto wao asipofanya vizuri wanaongea nao kwa lugha hasi na kuwaonesha kuwa hawawezi, mdomo wa mzazi ambaye kijana wake anamuona yeye ndo baba au mama, unamuumbia mwanafunzi au kijana husika hivyo kupoteza hali ya kujiamini,” alisema


Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents