Burudani

Amber Rose ampata mrithi wa Wiz Khalifa!

Mwanamitindo wa Marekani Amber Rose huwa hataki mchezo hata kidogo pale linapokuja suala zima la mahusianao.

Baada ya kukaa muda mrefu bila ya kuonekana na mpenzi mpya tangu alipoachana na mzazi mweziye Wiz Khalifa, mrembo huyo ameonekana kuingia katika mahusiano mapya na rapper 21 Savage.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Amber na Savage wameamua kufanya kweli baada ya wiki kadhaa kuzaniwa wawili hao wanamahusiano kwa kuonekana mara nyingi wakiwa wapo karibu, inadawa kuwa mpaka Savage anatarajia kwenda kumtambulisha Amber (33) kwa wazazi wake na familia yake kwa ujumla.

Amber Rose amemzidi mpenzi wake huyo mpya takriban miaka tisa, hata hivyo sio couple ya kwanza duniani kuzidiana umri, swali ni kuwa mrembo huyo ataweza kumsahau Wiz Khalifa ambaye mara kadhaa amekuwa akimpost mitandaoni?

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents