Habari

Mavuno ya misitu huchangia pato la taifa

Naibu waziri wa Maliasili na Utalii, Ramo Makani amesema mavuno ya misitu huchangia pato la taifa huku akisema mbao ni zao linaloiongezea serikali pato la taifa na kutoa ajira kwa wananchi.


Naibu waziri wa Maliasili na Utalii, Ramo Makani

Mhe. Makani amezungumza leo Bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Rita Kabati alietaka kujua mchango wa mauzo ya mbao kwenye pato la taifa.

“Ni Kweli kwamba mbao ni miongozi mwa mazao yanayochangia pato la taifa na pia kutoa ajira kwa wananchi zao hili zao hili linazalishwa kwa wingi katika wilaya ya Mufindi kutoka shamba la miti la serikali. Aidha kiasi cha fedha kinachopatikana kwa mwaka hutegemea kiasi cha Meta za ujazo kilichopangwa kuvunwa kulingana na mpango wa uvunaji kila shamba,” amesema Makani.

“Kutokana na mdororo wa uchumi miaka ya 1980 serikali ilibinafsisha viwanda vyake vikiwemo viwanda vya bidhaa za misitu vya serikali, ilibakiwa na jukumu la kuhifadhi misitu pamoja na kukuza miti katika mashamba yake, hivyo serikali huuza miti iliyosimama kwa wawekezaji binafsi ambao huvuna huchakata magogo kwaajili ya mbao, karatasi, nguzo na mazao mengine shuguli za uchakataji zinabaki kuwa shughuli za sekta binafsi kwa kuwa serikali haihusiki moja kwa moja takwimu za uchakataji.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents