Burudani

Asante Wema kwa kuniharibia penzi langu na Shilole – Nuh Mziwanda

Nuh Mziwanda amemtupia lawama Wema Sepetu kwa kitendo cha kuvujisha sauti aliyokuwa akimtongoza, kitendo ambacho muimbaji huyo amesema kimeutia doa uhusiano na mpenzi wake Shilole.

11326647_459262607579112_156873249_n

Nuh ambaye alikanusha taarifa za kumtongoza Wema, ameandika kwa urefu kwenye mtandao wa Instagram jinsi Wema alivyomletea shida.

Ameandika:

Nakupa hongera kwa kufanikiwa kutoa amani katika mapenzi yangu mimi Na zuwena’maana hukua na nia njema wewe pamoja na team yako’na hata kama ingekua kweli ungemfata pembeni zuwena na kumweleza kua bwana ako anantongoza na sauti zake hizi hapa’lakini ukaona sio ishu na kuachia mitandaoni’mradi kuniaibisha mimi pamoja na na huyo unaesema unampenda sana na ni shoga yako’kingine Wema umetongozwa na wangapi hapa duniani kwann usiweke Voic note zao?yani moja kwa moja umetaka kusambalatisha mapenzi yetu na now naona mnaanza kutumana kumtongoza shishi’well madam nakupa salute zako’najua unaishi kwa amani na raha ‘ila huku umekiwasha mpka mtu unakua hauna amani ya moyo na ukizingatia sijawahi hata kukaa na ww tukapga stor wala kuona undani wa mwili wangu’kipindi una kampeni uling’ang’ania sana niingie kwenye group yako ya whatsup for supporting you’kumbe unanichekea kinafiki na ulikua na mabomu yako umeyapanga kuyalipua ‘sawa mama angu ila mimi nimetoa ya moyoni mwangu kwako na naamini ujumbe utakufikia mana nimeshindwa kukaa na duku duku’sisi wote binadam na hatuna garantee ya kuishi’salute kwako kwa ulichofanya

Naye Wema amemjibu msanii huyo kwa maelezo hayo chini:

Naitwa Wema Sepetu na ntabaki kuwa Wema Sepetu… Iam Number One… Sina muda wa kubishana na watoto…Nina muda wa kufanya kazi na kwa sasa jicho langu limeelekea kwa Wanyaturu wangu Singida na kwenye siasa yangu pamoja na kazi zangu za maana bila kusahau entertainment niliokuwa ninayo from 2006 … Kumbe wakati mi nimelala nyie mnaandika Instagram… Ntapata dhambi kugombana na watoto wadogo-ambao nimewazidi sio pesa tu hadi dhambi pia nimewazidi…. Mstafute kick kupitia jina la Wema jamani… Jitume, amka, usibweteke, fanya kazi…. Umarioo mwisho Chalinze maana Dar wote tuna Hustle… Ama nene…. #WemaAbrahamSepetu#NumberOne#KibokoYao… Nimemaliza… Good morning everyone….!!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents