Burudani

Natamani Nimsimamie Barnaba Hata Miezi Sita – Said Fella

Meneja wa TMK Family pamoja na Mkubwa na Wanawe, Said Fella amesema kuwa anatamani angepata nafasi ya kufanya kazi na muimbaji Barnaba japo kwa miezi sita.

B n F

Fella ambaye amevumbua vipaji vya vijana wengi wa Temeke wakiwemo Yamoto Band, amesema hayo katika post ya kumpongeza Barnaba aliyekuwa akisheherekea siku yake ya kuzaliwa weekend iliyopita.

“Kuna vitu vya kulazimishwa lakini sio kuonyesha hisia mimi msanii wangu katika madogo walio chipukia wakati mh JAKAYA mrisho KIKWETE yupo madarakani ni uyu mwanangu barnaba mtoto wa kaka ruge muttahaba wakati anakivumbua nilisema ili zao akubahatisha hii ni nguzo moja muhimu ya kuta ya Tht na pia natamani boss ruge aniachie uyu kijana miezi sita najua yatafanyika mapinduzi ya hatari Leo ana kumbuka siku yake ya kuzaliwa happy birthday mwanangu barnaba mtoto wa kaka” aliandika Fella Instagram.

Mfano wa kile Fella anachotamani kukifanya kwa Baranaba, ni kama pale aliposaini na Shaa na kumbadili kutoka kufanya muziki wa ‘kishua’ hadi ‘kiswazi’, na kutoa wimbo wa ‘Sugua Gaga’ ambao video yake hadi sasa ina views 19,605,962 Youtube ambazo Shaa hakuwahi kuzipata katika video zake zote zilizopita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents