Burudani

Madee ajivunia kuisadia mengi jamii ya Manzese

Rapper Madee amesema anajivunia kwa kuhusika kwa ukaribu katika kutatua baadhi ya kero za wananchi wa Manzese anakojulikana kama Rais!

Madee2

Madee ameiambia Planet Bongo ya EATV kuwa wananchi wamemkubali kwa uwezo wake wa kupeleka ujumbe sehemu na ukasikilizwa mara moja tofauti na wananchi wa kawaida.

“Nimetatua kero za wananchi wa Manzese, watu waliweza kuwakilisha matatizo yao na nikayapeleka katika vyombo husika na yakatatuliwa,” alisema.

“Waliamini mimi kama mimi naweza kusikilizwa mapema tofauti na watu wa kawaida. Kama sasa hivi unavyoona Manzese ipo safi, watu zamani walikuwa wanaogopa kusema kwamba wao wanaishi Manzese, mimi ndio mtu wa kwanza kusema natokea Manzese na kukubali hali tuliyokuwa nayo. Kwahiyo wao wakaona mimi waniite rais, atakayekuja mwingine labda atakuwa waziri,” aliongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents