Habari
Askofu Kakobe aitwa Idara ya Uhamiaji
Askofu Mkuu wa Kanisa Full Gospel Bibble Fellowship, Zachary Kakobe amesema kuwa ameitwa kuhojiwa na Idara ya Uhamiaji siku ya Jumatatu.
Akiongea na Mwananchi, leo April 7, Zachary amesema kuwa ataitikia wito huo.
“Wamesema wananiita kwasababu ya mahojiano hivyo nitakwenda tu hakuna shida. Wameniita uhamiaji mkoa wa Dar es salaam,” amesema Kakobe.