Habari

Askofu Kakobe kuchunguzwa na TRA, ni baada ya kudai ana fedha kuzidi serikali

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema itamchunguza kiongozi wa Kanisa la Gospel Bible Fellowship Church (GBFC), Askofu Kakobe kufuatia kauli yake iliyodai ana fedha nyingi kuzidi serikali.

Akizungumza leo Dar es Salaam na waandishi wa habari Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere amesema Tanzania kuna matajiri wengi ambao wanalipa kodi lakini hawana fedha za kuizidi serikali hivyo wameshtushwa na kauli ya Askofu Kakombe ambaye hawana kumbukumbu/taarifa za ulipaji kodi wake.

“Hivyo basi sisi watu wa kodi tunataka tujiridhishe tu kuhusu suala la kodi linalomuhusu Askofu Kakoke na utajiri wake, kwa kuwa sisi ni wataalamu wa kodi basi tutafahama hicho kipato chake anachosema kama kinatokana na sadaka tu ama kuna shughuli nyingine za kiuchumi ambazo anazifanya tutajua,” amesema Kichere.

“Tunaelewa kwa mujibu sheria, taraibu na miongozo sadaka hazitozwi kodi lakini pia tunafahamu taasisi za dini huwa zina shughuli nyingine za kiuchumi, huwenda Askofu Kakobe na yeye kuna shughuli nyingine za kichumi huwa zinampatia hela kiasi kwamba akawa na pesa nyingi kuliko serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini kama ni sadaka pekee yake ni jambo la kushtua kidogo,” amesisitiza.

Kamishna Kichere amemaliza kwa kumtaka Askofu Kakobe kutoa ushirikiano kwa vijana wa mamlaka hiyo pindi watakapomtembelea ili kuweza kujiridhisha kuhusu suala hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents