Michezo

Atletico Madrid yaingia fainali ligi ya mabingwa barani Ulaya

Klabu ya soka ya Atletico Madrid imefanikiwa kutinga fainali ya klabu bingwa barani Ulaya kwa mara ya pili ndani ya kipindi cha miaka mitatu baada ya kupata bao la ugenini walipokipiga dhidi ya Bayern Munchen ya Ujerumani.

article-3571966-33CE558900000578-91_964x390

Mchezo wa Alianz Arena umemalizika kwa FC Bayern Munich kuibuka na ushindi wa goli 2-1, ila hiyo haikuisaidia kutinga hatua ya fainali, kutokana na kutolewa kwa aggregate ya goli 2-2. Magoli ya FC Bayern yalifungwa na Xabi Alonso dakika ya 31 na Robert Lewandowski dakika ya 74, huku goli la Atletico lilifungwa na Antoine Griezmann

33CDB13700000578-0-image-a-48_1462306857072

Matokeo ya jumla ya nusufainali hiyo yalimalizika sare 2-2 lakini Madrid wakasonga kwa kuwa na bao la ugenini.

33CDA0CE00000578-0-image-a-46_1462305817528

Sasa Atletico watakutana na mshindi wa mchezo kati ya Real Madrid na Manchester City utakaopigwa kesho dimbani Santiago Bernabeu katika fainali mjini Milan tarehe 28 Mei

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents