Burudani

Audio: MC Pilipili asimulia alivyoumbuka baada ya kupewa kazi kufanya UMC kwa Kiingereza kwa mara ya kwanza

Kwa MC Pilipili, kazi ya UMC kwenye sherehe mbalimbali hususan za harusi hakuzianza jana au juzi – ni kitambo.

12552461_1250016968346787_771982543_n

Alianza akiwa bado anasoma sekondari mkoani Dodoma ambako katika umri mdogo alikuwa ameshaupata umaarufu. Akiongea kwenye kipindi cha Chill na Sky, mchekeshaji huyo alikumbushia jinsi ambavyo aliumbuka baada ya kupewa kazi hiyo kwenye harusi iliyokuwa na ndugu kutoka Uganda ambako alilazimika kutumia Kiingereza kwenye kazi hiyo.

“Hiyo siku jasho lilinitoka,” anasema Pilipili. “Sababu naongea Kiswahili ‘jamani naombeni muingie’ wanasema ‘no unatakiwa uongee Kiingereza.”

Anasema alikitafuta Kiingereza kikagoma na akajikuta akiumbuka mbele za watu.

“True story, Dodoma Hotel hapo, nikaenda kwa DJ nikamuambia ‘mwanangu mimi naondoka.’ Hata hivyo amesema DJ alimsihi aendelea hivyo hivyo.

“Siku hiyo ilikuwa tete.”

Amesema baada ya kuona kuwa Kiingereza kimekuwa kigumu alijikuta akianza kuropoka kila neno lililokuja mdomoni bila kujali kama anaeleweka ama lah.

Hata hivyo waliohudhuria walihisi kuwa mchekeshaji huyo alikuwa akifanya makusudi na kuwavunja mbavu hivyo hivyo.

Sikiliza kipindi hicho hapo chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents