Habari

Audio: Nash MC awachana mashabiki wa hip hop Tanzania, awaita vigeugeu

Rapper wa Tamaduni Musik, Nash MC amesema anashangazwa sana na mashabiki wa Hip Hop Tanzania hasa wakati wa tuzo za KTMA zinazohusiana na hip hop. Amesema alishangaa kuona baadhi ya mashabiki wanalalamika kuwa Nay wa Mitego na Kala Jeremiah hawakustahili kupata tuzo ambapo amesema wengi wanaolalamika hawajui lolote kuhusu hip hop.

391513_524883240902995_1858787865_n

Akiongea na The Jump Off ya Times FM, Nash amesema, “Hawa wote wanaosema huyu hakustahili huyu amestahili, hivi vitu wanavifahamu? Tukianza kukaa kuweka mjadala utakuta vichwani mwao wako shallow, yaani hawana lolote ni kama tu wanalaumu.

Mimi Nash MC, Nikki Mbishi, One utakuta huko mtaani watu hapa wanatusifia sisi na hawanunui kazi zetu lakini wanatusifia ‘Nash MC ndio hip hop ya ukweli’ lakini Nash MC ana mixtape tatu sasa hivi mtaani lakini mtafute huyo mtu muulize unayo hata moja’ hana. Na akipewa Nay wa Mitego wanasema huyo sio hip hop, sasa wewe una support wapi? Waacheni machizi wachukue tuzo unakuwa ni kama wivu sasa, sasa huku sisi hutusupport na wale jamaa huwasupport sasa unasupport wapi?”

Msikilize zaidi hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents