Burudani

AY aeleza kwanini wasanii wakongwe wanashindwa kufanya vizuri

Msanii mkongwe wa Hip Hop Ambwene Yesaya ‘AY’ amesema wasanii wengi wakongwe wameshindwa kufanya vizuri kwenye muziki wa sasa kutokana na kushindwa kubadilika na kwenda kisasa.
Ay

Akizungumza katika kipindi cha Mkasi TV Jumatatu hii, AY alisema mabadiliko ni muhimu kwa kila msanii anayehitaji kwenda mbali zaidi.

“Kuna aina mbili za kupokea maoni kutoka kwa mashabiki, mtu anaweza akakwambia oya AY ulivyochana kwenye Raha Tu baki pale pale, sasa kuna artist wengine wanachukua vilevile bila kujua muziki una badilika kutokana na wakati,” alisema AY.

“Maisha ya binadamu sio kwenye muziki tu, hayawezi kwenda bila kubadilika. Kwahiyo wasanii hawapendi kubadilika, akishachukua maoni anayashikilia hapo hapo basi na yeye anabaki hapo hapo. Alianza kuimba nyimbo ya aina fulani basi atashikilia hapo hapo, hicho ndicho kinachowakosti, kwahiyo unamkuta mtu anaanza kulaumu media bila kujua hata media zinaenda na mabadiloko,” alisema AY.

AY kwa sasa anafanya vizuri na video ya remix ya wimbo Zigo ambayo amemshirikisha Diamond Platnumz.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents