Michezo

Azam FC yabadili mfumo wa uendeshaji na kuwa Kampuni

Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC imeingia kwenye mfumo wa Kampuni kwenye uwendeshaji wake na hivyo kuanzia sasa kutambulika rasmi kama Azam FootBall Club Company hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa timu hiyo, Nassor Idrissa.

Akizungumza kupitia Azam Tv, Mkurugenzi huyo wa timu ya Azam amesema kuanzia msimu ujao wa ligi klabu hiyo itatambulika kama Kampuni.

Azam kuwa Kampuni ni kwasababu ijulikane kwakuwa inathamani zake na zinatambulika kisheria na Serikali lakini pia kufahamika nani anatudhamini.

Kwahiyo klabu yetu msimu jao itakuwa ni Kampuni kwakuwa mambo mengine Serikalini yameshakamilika.

Azam FC msimu uliyopita imefanikiwa kumaliza kwenye nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara baada kwakuwa na pointi 58 huku ikiishusha Yanga hadi nafasi ya tatu kwakuwa na alama 52.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents