BurudaniHabari

Babu Tale: Ntalipia tiketi za wasanii 7 kwenda AFRIMA Marekani, watakaowahi kupata VISA

Kupitia ukurasa wa Instagram wa meneja huyo wa Diamond Platnumz na mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki ameandika kuwa:

 

“TWENDENI AFRIMMA.

Kwa sasa Muziki wetu umekua na kuifikia Dunia, ndio maana Wasanii wetu wameendelea kuchaguliwa kuwania tuzo mbali mbali kubwa ikiwepo hizi tuzo za AFIMMA @afrimma .

Tuzo hizi zitafanyika nchini Marekani mwaka huu 2022. Kwa kutambua umuhimu wa kuwakilisha nchi yetu, uwepo wangu kwenye tasnia ya muziki kwa muda mrefu na dhima ya kukuza sanaa yetu, nadhamiria kuhangaikia tiketi Saba za Wasanii waliochaguliwa kuwania tuzo hizi. NB: Hatakaewahi kupata VISA ndiye atakaewahi kupata ticket.

Hivyo niombe Baraza la Sanaa Tanzania @basata.tanzania(BASATA), kusaidia upatikanaji wa VISA za Wasanii waliochaguliwa kwani wote wanabarua za mwaliko.

Tuzo hizi ni muhimu kwa ukuaji wa muziki wetu na kulitangaza Taifa letu kwenye kile alichokianzisha Mheshimiwa Rais wetu cha kuvuta watalii nchini. Hii ikawe sehemu ya kila msanii shiriki kuizungumzia Royal tour akiwa huko nchini Marekani #theblackgodfather#malengo #theroyaltytour”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents