Burudani

Baby J adai changamoto hazijawahi kumkatisha tamaa kufanya muziki (Audio)

Baby J amesema changamoto anazopitia kila siku, hazijawahi kumkatisha tamaa ya kufanya muziki.

Akiongea na Bongo5, muimbaji huyo anayetokea Zanzibar, amedai kuwa alizaliwa na kipaji cha kuimba na wala hakuukuta muziki, hivyo kamwe hatorudi nyuma.

“Ni ngumu kukataa tamaa sababu naweza kufanya muziki wa aina yoyote na naweza kufanya chochote so siwezi kukataa tamaa,” amesema.

“Chochote kitakachotokea mbele yangu najua ni mapito tu lakini baadaye lazima nitulie nifanye kazi. Lakini haijawahi kuniijia akili ya kukata tamaa sababu sijaona kitu chochote kinachoweza kunikatisha tamaa mpaka sasa hivi, vitu vyote nahisi naweza kuvifanya,” amesisitiza.

Muimbaji huyo anadai kuwa sababu ya kuwa kimya ni mambo ya binafsi ya kifamilia yaliyokuwa yamembana na kwamba hivi karibuni ataachia kazi mpya. Kwa sasa yupo chini ya usimamizi wa Mkubwa na Wanawe ya Said Fella.

Baby J amewahi kufanya vizuri na nyimbo kama Bwashe aliyomshirikisha Alikiba, Bomoa Bomoa aliyomshirikisha Bob Junior, Moyo Wangu Umechoka aliomshirikisha Pasha, Nimempenda Mwenyewe na zingine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents