Balozi Mwambulukutu aporwa Afrika Kusini

BALOZI wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Emmanuel Mwambulukutu Ijumaa usiku alishambuliwa na majambazi, kujeruhiwa na kuporwa gari, simu ya mkononi, vito vya thamani na mali kadhaa.



Balozi Emmanuel Mwambulukutu


BALOZI wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Emmanuel Mwambulukutu Ijumaa usiku alishambuliwa na majambazi, kujeruhiwa na kuporwa gari, simu ya mkononi, vito vya thamani na mali kadhaa.


Chanzo chetu cha habari kinasema hivi sasa Balozi Mwambulukutu kalazwa Pretoria East Hospital kwa matibabu na uchunguzi umeonyesha uvimbe wa damu kichwani.
Tukio la uvamizi na uporaji lilitokea jijini Pretoria nyumbani kwa Dk Mlosi ambako Balozi Mwambulukutu na mkewe walikwenda kuhudhuria sherehe.


Majira ya saa tatu usiku, wavamizi waliruka ukuta na kuingia ndani ya nyumba ya Dk. Mlosi ambapo Balozi Mwambulukutu na mkewe ni baadhi ya waliokuwa wakihudhuria sherehe.
Watu hao wanaosadikiwa kwamba ni majambazi waliwafunga kamba watu wote waliokuwepo na kuamuru watoe simu za mkononi, saa na vito vya thamani na kisha kuendelea kuburudika kwa vinywaji na vyakula.


Baada ya kukusanya vitu vya thamani walimtaka afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Chris Sungura awapatie funguo za gari lakini ikashindikana kulitoa sababu lilikuwa limezibwa na gari la balozi.


Kulitokea mabishano pale walipomtaka Balozi Mwambulukutu awape funguo za gari lake na walipochukua funguo aliwaambia, “God Bless You”, kauli iliyoelekea kuwakera na kumpa kipigo kikali kilichoendana na mateke ya nguvu.


Licha ya balozi, mkewe nae alijeruhiwa kwa kitako cha bunduki na kupata majeraha yaliyosababishwa ashonwe kichwani na Sungura amepata jeraha jichoni.


Hata hivyo, gari la balozi lilipatikana baadae katika maeneo ya Mamelodi baada ya polisi wa Afrika Kusini kumtwanga risasi za miguu mmoja wa watu hao wanaosadikiwa kuwa majambazi.
Balozi Mwambulukutu amekuwepo nchini Afrika Kusini kwa wadhifa huo tangu 1999.


Source: Haki-Hakingowi

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents