Habari

BASATA lamfungia Rosa Ree miezi 6 kutojihusisha na muziki

Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) limemfungia miezi 6 msanii wa kike wa muziki wa hip hop hapa Tanzania, Rosa Ree kutojihusisha na shughuli zozote za kimuziki kwa makosa matatu likiwemo la kuachia video inayokiuka maadili ya kitanzania.

Related image
Rosa Ree

Akithibitisha taarifa hizo, Kaimu Katibu Mkuu Mtendaji BASATA, Onesmo Kayanda amesema kuwa msanii huyo pia amepigwa faini ya Tsh. milioni 2 kwa kosa la kufanya kazi za sanaa nje ya nchi bila kibali kutoka BASATA kama sheria inavyotaka.

Wimbo huo  wa ‘Vitamin U’ uliomponza Rosa Ree, Ameshirikishwa na msanii mwenzie kutoka Kenya, Timmy Tdat.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents