Burudani

Belle 9 aanzisha kampuni yake, inaitwa ‘Vitamin Music’

Msanii wa Morogoro, Belle 9 ameanzisha kampuni yake ya muziki iitwayo Vitamin Music.

10957307_642444542526075_1548043076_n

Akizungumza kwenye kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds TV, Belle 9 ambaye kwa sasa amehamia jijini Dar es Salaam alisema kampuni yake ndio itasimamia muziki wake na kuhakikisha unakuwa bora na kufika mbali.

“Nilikuwa nawaza muda mrefu kuwa na kampuni yangu ya ‘Vitamin Music Company’ lakini bahati nzuri nimepata washauri, nimekaa nao chini na kushauriana kampuni inahitaji equipment gani. Kwa sababu nilikuwa na idea lakini nilikuwa sijapata watu sahihi wa kuniongeza kwenye suala hili. Nimejipanga vizuri kama nilivyokwambia sasa hivi kazi zangu haziendi tena kama Belle 9, inafanya kama Vitamin Music Company.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents