Burudani

Enrico aeleza faida na hasara za kuwepo watayarishaji wengi wa muziki

Mtayarishaji mkongwe wa muziki hapa nchini, Enrico Figueiro wa studio za Sound Crafters, amezitaja faida na hasara zilizojitokeza kutokana na kuongezeka kwa watayarishaji wa muziki.

enrico

Enrico amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio kuwa wasanii wamenufaika zaidi lakini muziki umeshuka kiwango.

“Watayarishaji wa muziki wa sasa wengi ni vijana na hali ya computerized imekuwa rahisi kwao. Tofauti na sisi tulivyoanza mwanzo ambapo tulikuwa hatutumii computer na tulikuwa tunatumia analogue tools. Ndio maana sasa hivi vitu vingi vinaandaliwa kiurahisi,” alisema.

“Naweza kusema watayarishaji kuwa wengi imekuwa bora zaidi kwa sababu watu wamekuwa na access ya kurekodi kila sehemu kwa bei tofauti. Lakini kama wanataka viwango vyenyewe sidhani kama wanaweza kupata vile viwango vyetu vya zamani ambavyo tulikuwa tunaproduce sisi.”

Enrico ni miongoni mwa watayarishaji wenye tuzo nyingi za Kilimanjaro japo amekuwa akizipata kwa kutayarisha zaidi nyingi za Taarab.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents