Habari

Polisi watoa shavu kwa Vijana

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Camillus Wambura ametangaza nafasi za ajira kwa vijana wenye elimu ya Shahada, Stashahada, Astashahada, kidato cha nne ambao wana umri wa chini ya miaka 30.

Katika tangazo la ajira alilolitoa muda mfupi IGP Wambura amesema Vijana wenye elimu ya Shahada na Stashahada wanapaswa kuwa na umri kati ya miaka 18-30 wakati wenye elimu ya chini ya hiyo wawe na umri kati ya miaka 18-25.

Waombaji wa kidato cha nne wanapaswa kuwa na ufaulu wa daraja la kwanza hadi nne na wenye elimu ya kidato cha sita wawe na ufaulu wa daraja la kwanza hadi la tatu.

Vilevile, muombaji anapaswa kuwa na urefu usiopungua futi 5’8 kwa wanaume na kwa wanawake Futi 5’4 kwa wanawake.

Masharti mengine muombaji hapaswi kuwa ameoa au kuolewa ama kuwa na mtoto na awe hajawahi kutumia dawa za kulevya, pia muombaji hapaswi kuwa na alama za kuchorwa mwilini (Tattoo).

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

cc: Polisi Tanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents