Habari

Belle 9 azungumzia issue ya kutumia vionjo vya wimbo wa Saida Karoli kwenye wimbo wake ‘Give It To Me’ (Video)

Msanii wa muziki kutoka Vitamin Music Group Limited, Belle 9 amefunguka na kuzungumzia issue ya kutumia vionjo vya wimbo ‘Maria Salome’ wa Saida Karoli katika wimbo wake mpya ‘Give It To’ Me ambao umetoka weekend hii.

Akiongea na Bongo5 muda mchache baada ya uzinduzi wa video ya wimbo huyo, Belle 9 amedai wazo la kutumia vionjo vya wimbo huo alianza nalo toka zamani na sio kwa sababu Diamond na Darassa amefanya hivyo.

“Hata ukitoa wimbo iliokamilika huwezi kukataza comment ambazo zipo negative,” alisema Belle 9. “Kwa hiyo mimi niliuandika huu wimbo muda mrefu, G-Nako ni msanii mkubwa ana heshima, siamini kwamba mimi na G-Nako tukae studio tufanye kitu ambacho kimeshafanywa hicho ni kitu ambacho hakiwezekani,”

Aliongeza, “Lakini niwatoe hofu watu ambao walikuwa na maswali, Saida Karoli ni msanii mkubwa. Mimi niliuandika huu wimbo muda mrefu nikaenda studio kurekodi na G-Nako. Lakini wakati zinatoka project zao nilikuwa najisikia vizuri kumbe nimewaza katika ushindi kwa sababu zote zimefanya vizuri. Kwahiyo mimi ni mmoja kati ya watu ambao walifikiria hivyo, tena usishangae ukakuta kuna watu wengine wana ngoma nyingine nyingi wanafikiria kuweka hiyo copy. Kwahiyo ni kama appreciation ukimuongelea Saida kahuna mtu ambaye hajuhi uwepo wake,”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents