Benki ya NMB yashinda tuzo mbili za huduma bora Tanzania (+ Video)

Benki ya NMB yashinda tuzo mbili moja ikiwa ni Umahiri kwa miaka 9 mfululizo kupitia jarida la EURO MONEY kutokana na utoaji wake wa huduma kwa Watanzania.

Akiongea na wana habari Ruth Zaipuna ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB amesema kuwa:- NMB imeshinda tuzo nyingine ya Benki bora Tanzania kwa huduma binafsi na biashara za kati kwa mwaka 2021 kupitia jarida la Global Benking and finance ambalo linaaminika katika kufanya tafiti za Kibenki.

Majarida yote hayo makao makuu yake ni London nchini Uingereza, vigezo walivyozingatia ni pamoja na UFANISI NA UTENDAJI KWA UJUMLA, MKAKATI WA HUDUMA ZA KIJITALI, HUDUMA JUMUISHI ZA KIFEDHA, USALAMA WA HUDUMA ZA KIMTANDAO (CYBER SECURITY) NA MTAJI WA BENKI na vigezo vingine.

Baada ya hapo Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa NMB George Mulamula alizungumza kidogo na wana habari kabla ya kukabidhiwa tuzo hizo.

Related Articles

Back to top button