Mitindo

Best Off: Juma Jux anapoirudisha heshima ya old fashion

Mambo vipi! nakukaribisha katika ulimwengu wa mitindo ambapo huwa tunakuleta habari mbalimbali za mitindo, kama ilivyo ada yetu kila Jumapili ya mwisho wa mwezi kukuleta watu maarufu waliofanya vyema katika mitindo na leo tunamtazama Juma Jux katika uvaaji wake matata sana.

Jux ambaye ni msanii wa RnB, Bongo ameonekana kuwa na ushawishi haswa kwa vijana kutokana na mikato yake matata ambayo ilikuwa ikivaliwa zamani lakini kutokana na ubunifu wake na manjonjo yake nguo hizo zimeonekana kuvutia zaidi kwa sas kutokana na jinsi anavyoweza kupangilia.

Vile vile msanii huyo amekuwa akitumia mikato inato treand sasa kuchanganya na mikato yake hiyo. Najua unaweza kushangaa napozungumzia mikato ya zamai ni ipi, mikato hiyo ya zamani ni suruali kubwa anazovaa ambazo kwasasa zinaazna upa kurejea upya katika soko.

Yes!! Jux anastahili kupewa Best Off kutokana na jinsi anavyuoweza kuteka soko la mitindo na jinsi anayoweza kucheza vyema na rangi za nguo hizo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents