Habari

Bomu laua watu watatu Arusha

Watoto watatu waliokuwa wakichunga ng’ombe katika Kijiji cha Nafco, wilayani Monduli mkoani Arusha wamefariki dunia papo hapo baada ya kulipukiwa na bomu walilokuwa wakichezea.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo.

Tukio hilo limetokea siku ya Ijumaa jioni ya tarehe 15 Septemba mwaka huu katika Kijiji cha Nafco kilichopo Kata ya Loksale wilayani Monduli mkoa Arusha, eneo ambalo hutumiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa mazoezi.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, Julius Mhale amesema watoto hao wanatarajiwa kuzikwa kesho Jumatatu.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amethibitisha tukio hilo na kuahidi kutoa taarifa rasmi baadae.

Chanzo: Mwananchi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents