Habari

Bonta: Utazomewa ukisema mimi sio conscious, avunja ukimya kwa ngoma mpya ‘Mtaani watu Buuu’ (Audio)

Rapper wa kampuni ya Weusi, Bonta, amevunja ukimya kwa kuachia wimbo mpya, ‘Mtaani watu Buuu’. Katika wimbo huo aliomshirikisha G-Nako na kutayarishwa na producer Mona Gangster, rapper huyo anajaribu kuwakumbusha kuwa watu bado ni conscious rapper na kama ukibisha watu watakuzomea.

480242_395501530523359_384316722_n
Bonta akiwa na Adili

“Unaposema mimi sio conscious mtaani watu buuu, ongea ongea tu mafumbo uoga, sikio halipimi neno kama ulimi uonjavyo mboga, kama kiporo hakiitaji moto mwingi basi sihitaji nguvu kupambana na hawa ‘wabishi’, anarap Bonta.

Bonta ameendelea na kuwapa dongo Ali Kiba na Ommy Dimpoz akichana: Ukisikiliza Dushelele mimi ntarewind Propaganda na ukipozi Nai Nai mimi ntafanya Manuva kwenye posa kama Langa.”

Usikilize hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents