HabariMichezo

Breaking: Manchester United watangaza kumalizana na Ronaldo

Cristiano Ronaldo anatarajiwa kuondoka Manchester United kwa makubaliano ya pande zote mbili mara moja kufuatia mahojiano yake na Piers Morgan.

United ilitoa taarifa ya maneno 67 Jumanne jioni ikitangaza kuwa wamefikia makubaliano na mchezaji huyo kusitisha mkataba wake.

 

Mahojiano ya Ronaldo kwenye TalkTV – yaliyoonyeshwa katika sehemu mbili Jumatano na Alhamisi wiki jana                                                                                                   Humheshimu.

 

Ronaldo pia alidai wanachama wa uongozi wa United wanajaribu kumfukuza Old Trafford na walimtilia shaka aliposema hangeweza kuhudhuria pre-season kwa sababu binti yake alikuwa mgonjwa hospitali.

United walisema watazingatia majibu yao kwa maoni ya Ronaldo “baada ya ukweli kamili kuthibitishwa” na sasa wameamua kuachana na mshindi huyo mara tano wa Ballon d’Or.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents