Habari

Chama tawala Nigeria wakusanyika kumchagua mgombea urais 

Zaidi ya wajumbe 2,000 wa chama tawala cha Nigeria cha All Progressive Congress wamekusanyika katika mji mkuu Abuja kwa lengo la kumchagua mgombea atakayewania kuiongoza nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika.

Wajumbe wa chama tawala nchini Nigeria cha All Progressive Congress APC wamekutana usiku wa kuamkia leo kushiriki kura ya mchujo ya kumchagua mgombea atakayepeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao ili kuchukua nafasi ya rais Muhammadu Buhari.

Msemaji wa Buhari Garba Shehu amesema rais huyo hana mgombea anayempendelea kutoka chama hicho tawala. Wagombea waliojitokeza kuwania tiketi ya chama hicho ni pamoja na gavana wa zamani wa Lagos Bola Tinubu, Makamu wa Rais Yemi Osinbajo, waziri wa zamani wa uchukuzi Rotimi Amaechi na kiongozi wa bunge la seneti Ahmad Lawan.

Buhari ambaye kisheria amezuiwa kugombea tena wadhfa huo, anamaliza muhula wake mwaka 2023 baada ya miaka minane madarakani, na hivyo kusababisha uvumi juu ya mgombea atakayemuunga mkono kama mrithi wake.

Kiongozi huyo wa Nigeria aliwasili katika kituo cha mkutano cha Eagle Square mapema jana jioni kabla ya zoezi la kumchagua mrithi wake kuanza.

Buhari ametumia siku kadhaa kabla ya kongamano hilo la chama tawala akijaribu kutuma ujumbe wa umoja chamani baada ya kuibuka mirengo tofauti juu ya mgombea anayestahili kupeperusha bendera ya chama katika uchaguzi wa urais mnamo Februari mwakani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents