Burudani

Chanzo cha bifu ya Taylor Swift na Katy Perry ni kuchukuliana dancers

Kwa mujibu wa Taylor Swift, Katy Perry ni mwizi na hiyo kwa mujibu wa mtandao wa TMZ ndio chanzo cha uadui wao. Uadui wa wanamuziki hao wa kike ulianza baada ya dancers watatu wa Taylor kuungana na na Katy kwenye ziara yake.

page

Taylor alihisi kusalitiwa kwakuwa alikuwa amezoeana mno na dancers hao kiasi cha kuwachukulia kama watu wa familia yake. Hata hivyo TMZ imedai kuwa dancers hao watatu walikuwa wakifanya kazi na Katy awali lakini baada ya ziara yake kumalizika miaka kadhaa iliyopita walihitaji kupata kazi nyingine. Hivyo walijiunga na Taylor kama dancers katika ziara yake.

Inadaiwa kuwa dancers hao walimwambia ukweli Taylor kuwa hawakutaka kusaini kufanya ziara nzima bali ni siku 30 peke yake kwakuwa walikuwa wakimkongoja Katy arejee ziarani. Baada ya Katy kurejea tena kwenye ziara ndipo walipoomba kuondoka lakini Taylor alichukia na kuwafuza mara moja.

Yote hayo yalitokea mwaka uliopita lakini inasemekana kuwa Taylor alikuwa na kinyongo kilichomfanya aandike wimbo uitwao “Bad Blood” akimponda Katy kwa kumsaliti. Iligeuka kuwa vita kamili baada ya Katy kujibu kupitia Twitter kwa kumuita Swift … Regina George ndani ya nguo za kondoo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents