Burudani

Chemical na Pink kuwafuata Rostam, MoCo

Wasanii wa muziki Bongo, Chemical na Pink wamefunguka kuunda umoja wao/kundi.

Marapa huo  wameiambia Ladha3600 ya E Fm kuna uwezekano wa kufanya hivyo kwani ni kitu kizuri kibiashara.

“Tunaweza kuendelea kufanya kwa sababu so far hii  ngoma ya Achana na Mimi inaenda vizuri na unajua imekusanya mashabiki wa Chemical na Pink, kwa hiyo kibiashara ni nzuri pia, hivyo haitakuwa mbaya ukisikia track nyingine ya Chemical  na Pink,” amesema Chemical.

Chemical na Pink kwa sasa wanafanya vizuri na ngoma inayokwenda kwa jina la Achana na Mimi.

Hivi karibuni wasanii wa hip hip Bongo wamekuwa wakiunda umoja wa kutoa ngoma pamoja, miongoni mwao ni Roma na Stamina (Rostam), Moni na Country Boy (MoCo).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents