Burudani

Chin Bees aipa tano ‘Kababayee’ kwa mwaka 2017

Msanii wa muziki Bongo, Chin Bees ameitaja ngoma yake ya Kababayee kama ngoma yake iliyofanikiwa zaidi kwa mwaka huu.

Chin Bees ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa ngoma hiyo imeweza hata kumtangaza nje ya nchi.

“Mwaka 2017 umekuwa mkubwa, kwanza ninachoshukuru ngoma yangu ya Kababayee imeweza kushika namba moja katika vituo vikubwa vya station, huko nje ya nchi, ni kitu kikubwa sana kimeweza kumtambulisha Chin Bees,” amesema.

“So ni kitu kikubwa sana ambacho naweza nikamshukuru Mungu na 2017 ndio kitu ambacho nimekifanya, so much love kwa mashabiki wangu,” ameongeza Chin Bees.

Ukiachilia mbali ngoma ya Kababayee kwa mwaka huu Chin Bees ameweza kutamba na ngoma kama Nyonga Nyonga na Pepeta.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents