Chris Brown aburuzwa tena mahakamani kwa kumpiga demu wake

Baada ya kesi kubwa ya kumpiga aliyekua mpenzi wake wa wakati huo, Rihanna, Chris Brown ameburuzwa tena mahakamani kwa tuhuma zile zile lakini zikiwa ni kwa aliyekua demu wake baada ya Rihanna, Karrueche Tran.

TMZ IMERIPOTI KWAMBA, siku ya birthday ya Chris brown ndio mahakama ilipomletea barua ya wito wa kufika mahakamani kuitikia kesi la shitaka la kumpiga aliyekua mpenzi wake, huku akiwa tayari na kesi nyingine ya kumpiga Rihanna.

Karrueche anatarajia kuonekana mahakamani kutoa ushahidi dhidi ya Brown kumpiga teke tumboni na kumsukuma kwenye ngazi na kusababisha yeye kuanguka na kupata majeraha.

Inasemekana mwanzoni, wakati wa kesi ya Rihanna, Chris alizongwa na matatizo mengi kisheria kiasi cha kuathiri muziki wake, na maisha yake ya ustaa kwa ujumla.


Kambi ya Breezy bado iko kimya kuhusiana na kesi hiyo mpaka sasa.

Related Articles

Back to top button