Burudani

Christian Bella ataja kitu ambacho hatokisahau maisha mwake

King of the best melody Christian Bella amefunguka na kutaja wakati mgumu ambao amewahi kuupitia na hatokuja kusahau kwenye maisha yake yote.

bella

“Ugumu wa maisha ni kitu cha kawaida kwangu. Kitu ambacho nimekipitia na kilikuwa kigumu kwangu pale niliposhuhudia live mke wangu anajifungua. Mwanzo waliponiambia atakapokuwa akijifungua nitatakiwa niwepo nikajua ni utani lakini siku ilipofika nilichanganyikiwa, walinivalisha mavazi na mimi kama daktari nikaingizwa ndani nikawa nashuhudia live,” amekiambia kipindi cha My Playlist cha Clouds TV.

“Hapo ndipo nikaandika wimbo wa ‘Nani Kama Mama’ niliuandika kwa uchungu mkubwa huku machozi yakinitoka wakati nipo hospitali,” ameongeza.

Kwa sasa muimbaji huyo anafanya vizuri na wimbo ‘Nishike’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents