Burudani

Christina Milian aeleza sababu ya kuachana na Lil Wayne

Hatimaye Christina Milian ameeleza sababu iliyopelekea kuachana na Lil Wayne baada ya kudumu kwa zaidi ya mwaka mzima.

christina-milian-focus-movie-premiere-in-los-angeles_1

Milian ametumia reality show yake kueleza chanzo hicho na inaonekana Weezy hakuwa mwaminifu. Milian anadai kuwa alifanya uchunguzi wake na kubaini kuwa mwanamke mmoja stripper alipiga picha kutoka kwenye nyumba ya Weezy.

Hakueleza kwa kina nini kingine alichogundua kati ya wawili hao.

“Sijawahi kumpenda mtu mwingine jinsi nilivyompenda Wayne, sio hata mume wangu wa zamani,” Milian alisema kwenye kipindi hicho na kudai kuwa waliachana kwa njia ya simu.

Pamoja na wawili hao kuachana bado wameendelea kufanya kazi na bado yupo chini ya Young Money.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents