Burudani

Country Boy ajiandaa kuachia mixtape mpya, ‘Kama Ulaya’

Rapper Country Boy amesema ataachia mixtape mpya hivi karibuni.

COUNTRYBOY1

Rapper huyo amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM kuwa mixtape hiyo ameipa jina, Kama Ulaya.

“Idea ya kuita mixtape ‘Kama Ulaya’ imekuja baada ya kuona mimi ni mtu ambaye nilikuwa nafanya mixtape za mbele yaani ngoma za wasanii wa mbele na zime-hit,” alisema. “Mimi nina uwezo wa kubadilisha ngoma yoyote na unaweza kuona kama mixtape ya Bobby Shmurda, Hot Nigga na Kendrick Lamar ambayo nilifanya kwa style zao zile zile na watu wakakubali uwezo wangu,” aliongeza.

“Sasa ndio umefika muda wa kuachia mixtape yangu ambayo nitakuwa na uhuru nayo na haki nayo nikimaanisha kila kitu kiwe changu. Kwahiyo nikaingia studio kwa Lufa na kuanza kurekodi ngoma 10 na bado tunaendelea lakini itatoka mwaka huu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents