Burudani

Mwimbaji wa Jamaica, Alaine aisifia ‘Never Ever’ ya Vanessa Mdee

Inatia moyo kuona jinsi muziki Bongo unavyozidi kupenya kwenye masikio ya mashabiki wa nje wakiwemo mastaa, hii ni kutokana na jitihada zinazofanywa na wasanii wa Tanzania wanaowekeza kufanya muziki mzuri na video kali.

Alaine TZ
Alaine alipotua Tanzania 2013

Baada ya mtangazaji maarufu wa Afrika Kusini, Bonang Matheba kuonesha kuukubali wimbo mpya wa Joh Makini aliomshirikisha AKA wa Afrika Kusini ‘Don’t Bother’ kwenye post ya AKA Instagram, mwimbaji mwingine wa Reggae kutoka Jamaica aliyewahi kuja Tanzania kwenye tamasha la Fiesta mwaka 2013, Alaine Laughton ameusifia wimbo mpya wa Vanessa Mdee ‘Never Ever’.

Alaine na Vanessa

Alaine alianza kwa kupost picha aliyopiga alipokuja Tanzania, akiwa na Millard Ayo, Vanessa Mdee na Mohombi kwenye studio za Clouds Fm, na kuandika “#fbf to TZ with my beautiful supertalented sista @vanessamdee , @mohombimusic and @millardayo #goodtimes #TZ #smile #hello #musicallyconnected #Jamaica #Africa #Tanzania #onelink”.

Vanessa alicomment kwenye post hiyo kwa kuandika “BTW LOOOOOVE YOUR HELLO REGGAE COVER” na ndipo Alaine alimjibu “I love ‘Never Ever’ it’s sooo my jam….#onrepeat#”

alaine vanessa

Alaine alitambulishwa vizuri Afrika Mashariki na Wyre aliyemshirikisha kwenye hit song yake ‘Nakupenda Pia’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents