Burudani

Country Boy adai anafanya jitihada kulirudisha kundi la ‘Mtu Chee’

Rapper Country Boy amesema kundi la muziki lililokuwa kimya kwa miaka miwili, Mtu Chee, linatarajiwa kurudi kwa kasi kubwa katika tasnia ya muziki.

11821164_1639903142954587_408394810_n

Kundi hilo linaloundwa na wasanii Boniventure Kabogo maarufu kama Stamina, yeye mwenye ambaye jina lake halisi ni Ibrahim Mandingo ‘Country Boy’ na David Genzi maarufu kama Young Dee linarudi baada ya maombi ya wadau mbalimbali wa muziki nchini.

Rapper huyo ameliambia gazeti la Mtanzania kuwa wameshaanza kurekodi kwa producer Rash Don katika studio ya Kiri Records, ili kurudisha upya kundi hilo lililowahi kutamba na wimbo ‘Mia’ uliotengenezwa na Manecky.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents