Burudani

K.O asifia kipaji cha Nahreel, asema beat zake ni ‘special’ (Video)

Rapper wa Afrika Kusini, K.O amesifia kipaji cha producer wa The Industry, Nahreel.

K.O ambaye yupo nchini kwa ziara ya siku mbili ameiambia Bongo5 kuwa beats za Nahreel ni ‘special’.

“Nahreel alinitumia beats kali sana, na nilimchezea pia AKA, tuna mpango wa kurekodi kwenye beat moja wapo ya zile alizonitumia,” amesema.

“Bila shaka album yangu ijayo naweza kuwa na nyimbo moja au mbili kutoka kwa mshkaji na wakati nipo hapa nitamtafuta na kuona kama naweza kupata zingine sababu napenda ukweli kuwa beat zake ni tofauti na zile nilizozea kutumia,” aliongeza.

“Zake hazisikiki kama beat za Kimarekani, zake hazisikiki kama beat za Afrika Kusini, zinasikika kama kitu fulani kikali na special kutoka kwenye upande tofauti wa dunia.”

Tayari K.O na Nahreel wameingia studio kurekodi wimbo na Weusi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents