Michezo

Dau la Philippe Coutinho lamkaribia Neymar

Klabu ya Liverpool imekataa ofa ya paundi milioni 113 kutoka kwa Barcelona ili kumsaini mchezaji wao raia wa Brazili, Philippe Coutinho.

Kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali vya habari, hii ni kwa mara ya tatu kwa Liverpool kuchomoa ofa ya kumuuza Coutinho kwenda Barcelona licha ya dau hilo huenda kuongezeka hadi kufikia paundi milioni 118.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazili ameonekana kuwa muhimu ndani ya Nou Camp hadi matajiri hao wa Hispania kuongeza dau nono kiasi hicho baada ya paundi milioni 72 nazile paundi milioni 90 za hapo awali kugonga mwamba.

Licha ya Liverpool kusisitiza kutomuachia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 katika dirisha hili la usajili lakini Meneja Mkuu wa Barca, Josep Segura mapema wiki iliyopita alisema kuwa wanakaribia kufikia makubaliano juu ya Coutinho.

Hata hivyo alipo ulizwa kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp juu ya maneno ya Meneja huyo wa Barca amesema kuwa “Hata sifahamu kwa nini watu wengine huzungumza hayo yanayozungumzwa.Wala simfahamu na wala hatujawahi kukutana,”alisema Klopp.

Kwa mujibu wa muandishi wa habari za michezo wa Sunday Times, Duncan Castles amesema kuwa habari za ndani ya klabu hiyo za kukataa kumuuza mchezaji huyo ni danganya toto na badala yake wanahitaji paundi milioni 137 sawa na dola ilioni 150 kiasi ambacho hata Borussia Dortmund walikihitaji kutoka kwa Barcelona ili kumuachia Ousmane Dembele.

Barca ipo katika wakatimgumu toka kumuuza mchezaji wao Neymar  kwenda PSG kwa dau lililoweka rekodi ya dunia ya paundi milioni 222 na huku ikikubali kipigo cha magoli 5-1 kutoka kwa mahasimu wao Real Madrid katika mchezo wa the Super Cup.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents