Habari

DC wa Ilemela Dkt. Lalika akoshwa na uwekezaji unaofanywa na Tigo Mwanza

Wakati maandalizi ya Tamasha kula Fiesta yakiendelea hapo kesho, Kampuni inayoongoza katika maisha ya kidijitali Tanzania,Tigo, leo imefungua duka jipya jijini Mwanza.Duka hilo litawafanya wateja wa kampuni hiyo kupata huduma zote kwa urahisi zaidi ndani ya eneo moja la Rock City Mall.

Duka hilo litatoa huduma zote muhimu kuanzia usajili wa namba za simu kwa alama za vidole, huduma za kifedha ‘Tigo Pesa’ na mauzo ya data na vifaa vya mawasiliano kama simu janja, router na modem kwaajili ya huduma yetu tuliyo zindua hivi majuzi iitwayo ‘Tigo Home internet’.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati amesema hatua ya kufungua duka hilo ni moja ya mkakati wa Tigo wa uboreshaji wa huduma na kuhakikisha zinawafikia wateja kwa wakati nchi nzima.

“Duka hili jipya litampa mteja wetu wasaa wa kutazama na kujaribu bidhaa mbalimbali kabla ya kuamua kufanya manunuzi.Hatua hii imekuja kufuatia maombi ya muda mrefu kutoka kwa wateja wetu waliokuwa wakihitaji uwepo wa duka letu kwenye jengo hili maarufu kibiashara hivyo tumekidhi mahitaji yao,”alisema Madati.

Awali akizindua duka hilo, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela,Mkoani Mwanza, Dkt.Severine Lalika alipongeza juhudi za Tigo katika kuwekeza rasilimali katika uboreshaji wa huduma na kuhakikisha zinakidhi viwango vya kimataifa.

“Huduma bora kwa wateja ni kitovu cha biashara na zaidi huwafanya wateja wajisikie wanathaminika na kuheshimiwa, Tigo wametekeleza jambo hili kwa vitendo kwa kufanya uwekezaji katika utoaji wa huduma zao jambo linalowapa utofauti wa kipekee sokoni,” alisema Lalika.

Kadhalika,duka hilo linakuwa la nne kufunguliwa mkoani humo huku likiwa na huduma mpya ikiwamo simu zinazotamba kwa sasa aina ya S3 na R7 pamoja na vifaa vya huduma za intaneti kwa makampuni maarufu kama ‘Tigo business’.

Maduka mengine matatu ambayo yanatoa huduma mkoani hapa ni pamoja na Mwanza kiosk-barabara ya Nyerere, Ukerewe shop-Wilaya ya Ukerewe, Sengerema shop-Wilayani Sengerema na Airport kiosk- Uwanja wa ndege wa Mwanza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents