Habari
Deni la Marekani kutawala Mkutano wa G7
Mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu kutoka kwenye mataifa saba tajiri ( G7 ) wameanza mkutano wao unaofanyika nchini Japan ambapo wanajadili kuhusu masuala muhimu ya Dunia.
Wasiwasi juu ya kiwango cha juu cha deni la taifa la Marekani umetawala mkutano kutokana na kwamba iwapo nchi hiyo itashindwa kulipa deni lake basi dunia itakumbwa na mtikisiko mkubwa wa kiuchumi.
Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen amesisitiza kwamba mojawapo ya vipaumbele vyake ni kutatua mgogoro wa deni unaolikumba nchi yake ambapo amelitaka bunge la Marekani kuongeza kikomo cha deni la taifa la dola trilioni 31.4 ili kuepusha hali ya kushindwa kulipa deni ambayo ikitokea itasababisha kuzorota kwa uchumi wa dunia nzima.