Diamond: Sikuwafundisha Harmonize na Rayavanny kupelekana polisi, washindane kwenye nyimbo

Akiongea katika kipindi cha Refresh kinachoruka Wasafi tv CEO wa WCB Diamond Platnumz ameeleza na kuonyesha kuchukizwa na mambo yanayoendelea kati ya msanii wake Rayvanny na aliyewahi kuwa msanii wa lebo hiyo Harmonize kupelekana Polisi.

Harmonize na Rayvanny kesi yao ipo Polisi kutokana na Harmonize kushtaki kuwa anachafuliwa kwa baadhi ya picha zake za utupu kusambaa mitandaoni.

Harmonize aliwashitaki wote waliohusika kusambaza hizo picha huku akiwashuku Rayvanny, Baba levo, Paula mtoto wa Kajala na Kajala mwenyewe.

Diamond ameongeza kuwa anachotaka kuona ni kusikia wananshindana kwenye kazi na sio mambo yasiyohusu kazi, huku akichomelea msumari wa mwisho kuwa yeye hakuwafundisha kupelekana Polisi, Sijafurahishwa kusikia wanapelekana Polisi, Waige mifano ya sisi kaka zao mfano mimi na Alikiba hatukuwahi kuepelekana polisi tulikuwa tunashindana kupitia kazi zetu tu.

Related Articles

Back to top button