Burudani

Director Rey: Muongozaji wa video za muziki na mpiga picha Mtanzania anayeiteka Afrika Kusini (Exclusive)

Kwa wanamuziki wa Tanzania, Afrika Kusini imegeuka kuwa kama Kingston, Jamaica ilivyo kwa wanamuziki wa reggae duniani. SA imekuwa sehemu inayotumiwa na wasanii wengi wakubwa kufanya video za ngoma zao.

tumblr_obg5q7qxbw1vb6yrxo1_1280

Lakini huko huko kuna muongozaji aliyeanza kujipatia umaarufu kwa uongozaji wa video za muziki hususan za hip hop. Jina lake la kazi ni Director Rey.

Nimefanya naye mahojiano ili kumfahamu zaidi.

Jitambulishe na utuambie umezaliwa wapi?

Jina langu kamili naitwa Ramadhani Said, mtoto wa kwanza wa kiume kwenye familia ya watoto 4. Nimezaliwa Tanzania, Dar es – Salaam wilaya ya Temeke. Nimelelewa na wazazi wote wawili mpaka elimu ya kidato cha 4 ambapo nilikataa kuendelea shule na kuanza kusomea colorist & computer engineer ndani ya South AAfrica kwa miaka 3. Miaka sita ya kukaa nje ya nchi imenifanya nikaze jembe kufikia kile ninachotamani.

Kwa sasa wengi wananifahamu kama “Director Rey” mshindi wa tuzo za 2015 Architect SA Film awards. Colorist I Visual storyteller na Photographer pia.

Afrika Kusini unafanya nini?

Nilikuwa mwanafunzi Cape Town, chuo cha Sanaa, Cape Town Creative Academ, nimemaliza 2014, nikafanya kazi pale UKZN TV mwaka mmoja, nikaacha na kuanza focus kwenye TV commercials, music videos & films. Kazi ya picha sikusomea hata kidogo ujuzi mwingi ni wa kutoka internet, ila music videos baada ya kufanya kazi na professional director wakati bado nafanya D.O.P tu wakanishauri nikamate shorty course pale Cape Town kwa miezi 6.

tumblr_obg85myak01vb6yrxo1_1280

Umeshafanya kazi zipi za video huko?

Kazi nyingi nimefanya kama DOP za wasanii wakubwa kabisa SA. Nimefanya pia na Masandi toka Cashtime LIFE. Na kwa sasa nimeshoot wimbo unaitwa BEEN THINKIN ni wimbo ambao uko juu sana now radio zote, blogs. Clubs wanaipa sifa, so nimeshoot hiyo ntaiachia premier kwenye matv na kwenye YouTube channel yangu.

Wasanii wa Tanzania wanaenda sana SA kufanya video zako, kuna yeyote amewahi kukutafuta?

Yes, wapo kama zaidi ya 4 ila nimeshafanya na Shilole – Say My Name. Nilipata kuonana na Shilole muda mfupi so nikafanya naye video. Mwingine anaitwa Mauzo – Dear God.

Una mpango wa kuuleta ujuzi wako Tanzania na kushoot video za wasanii wa hapa?

Miaka 6 ya nje ya nchi imenifanya nione thamani kubwa sana nikiangalia Tanzania ya sasa. Kwa sasa nina kiu ya kushoot ndani ya nchi yangu. Nataka kuwafanya wasanii wa nchi au ndani ya Africa kuja video zao kushoot Tanzania hiyo ndio plan.

Video zinafanyika Tanzania zina kasoro gani?

Kasoro zipo, mengi tu ila nafikiri muda unavyoenda tutajifunza vyema, kwa mfano mavazi ya asili, Tanzania hatutambuliki vazi letu la hasiri ni lipi… unaimba Kiswahili mavazi ya Nigerian, video nyingi tu ziko hivyo.

Ni mazingira gani yanafanya kufanya video SA yawe rahisi kwa msanii?

Ukijulikana na watu basi ni rahisi kupata chochote, kwa mfano mimi nikitaka gari watanipa kwa sababu profile yangu inaonekana na kazi wanaziona kwenye matv na internet, so ni mtu ambaye wanajua nafanya nini. Kingine wenyewe wanasapoti sana entertainment.

Ukitaka kuwasiliana na Director, mfollow Twitter au mcheck kwa email [email protected]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents